Pages

Pages

Pages

Friday, 11 April 2014

CHADEMA ARUSHA WAANZA KUWAFUATILIA MADIWANI


Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Wilaya ya Arusha kimeanzisha kampeni ya kufuatilia kazi na miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na madiwani wake lakini pia kutafuta madiwani vivuli kwenye kata ambazo zina madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM). 
Hayo yameelezwa mapema jana  na Katibu wa Wilaya wa Chadema,Marti Sarungi wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na miradi inayoendelea kutekelezwa chini madiani wa chsma hicho kwa Wilaya ya Arusha.
Sarungi alisema kuwa lengo halisi la kuwafutilia madiwani hao ni kuakikisha kuwa wanatekeleza ahadi ambazo walizitoa wakati wa kampeni ili kuweza kuondoa malalamiko na manunguniko yalioko kwenye jamii.
Alisema kuwa lakini mbali na kutekeleza ahadi hizo pia ni kuweza kuwajulisha wananchi kinachoendelea kwenye kata pamoja na miradi ambayo imetekelezwa na madiwani wa Chadema na hivyo kuondoa usiri mkubwa pamoja na ubatlifu wa fedha za umma ambao unafanywa na viongozi wa Jiji wasiokuwa waadilifu kwa umma.
“Tunataka miradi yote inayotekelezwa na madiwani wetu isiwe ni siri bali iwe wazi na hii itatusaidia sana hata kuwabana madiwani wenyewe ambao wakati mwingine wanajisahau tutawafutilia kichama hadi kimtaa na pia itaongeza hata nidhamu kwao," aliongeza Sarungi.
 Alisema kuwa kwenye kila mtaa kutakuwa na madiwani hata kama kata inaongozwa na CCM, TLP ambapo kwa sasa kwenye kata za viongozi hao zote kutakuwa na walezi ambao wanalenga kuwasaidia wananchi kwa misaada na hata ushauri hasa pale panapohitajika.
“Hata kama kata inaongozwa na chama kingine sisi pale tutaweka diwani kivuli ambaye ataweza kusaidia jamii ya pale kwa misaada yote inayohitajika lakini pia tutahakikisha kuwa kata zote za hapa Arusha mjini kutakuwa hakuna siri za miradi ya aina yoyote ile,” aliongeza Sarungi.
Sarungi alitumia nafasi hiyo kushauri uongozi wa Jiji la Arusha kuweza kuweka mikakati mbalimbali na endelevu ya kusafisha jiji la Arusha kwani oparesheni waliyoweza kuweka ya kuondoa nyumba na wafanyabishara wasio na ulazima kukaa katikati ya Jiji la Arusha ilikuwa ni nzuri ila bado Jiji ni chafu.
“Natumia nafasi hii kusema kuwa pamoja na kuwa kweli sasa jiji lipo mahali pake lakini bado linaonekana likiwa ni chafu sana nah ii ni changamoto kwa uongozi wa Jiji kuhakikisha kuwa wanaweka taratibu za usafi pamoja na sheria,kanuni, na taratibu maalumu za kuweza kuongeza sifa ya Jiji,” aliongeza Sarungi.

No comments:

Post a Comment