Pages

Pages

Pages

Sunday 20 April 2014

ADC: MUUNDO WA UTAWALA UNATUKOSESHA KATIBA

ADC: Muundo wa utawala utatukosesha Katiba
CHAMA cha Alliance For Democratic Change (ADC) kimesema msuguano wa muundo wa utawala unaondelea sasa unapaswa kumalizwa na wananchi kwa kura ya maoni.
Aidha, kimesikitishwa na namna Bunge la Maalumu la Katiba linavyoendeshwa wakidai kwamba limetekwa na vyama vya siasa badala ya kuwawakilisha wanachi.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili jana, Mwenyekiti wa ADC, Said Miraji, alisema wakati wanawasilisha maoni yao kwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, walipendekeza kuwa ifanyike kura ya maoni kabla ya bunge hilo kwa ajili ya kujadili hoja ngumu ikiwano ya muundo wa utawala.
“Baada ya kuona kwamba zitatokea sintofahamu kwa chama tawala na vyama vya upinzani ambavyo haviamini tulipendekeza katika tume kwamba suala hili lifanyiwe kazi kwa kuitisha kura ya maoni ya wananchi wote kabla ya bunge la katiba kuketi.
“Lakini nyote mtakubaliana na mimi kwamba kinachoendelea sasa bungeni ni matakwa ya vyama vya siasa… CCM wanasema serikali mbili, UKAWA wanasema serikali tatu hata kuamua kutoka bungeni.
“Tofauti hizo ndiyo zimepoteza uhalali wa msingi wa rasimu ya katiba ya wananchi wanayoitaka na badala yake imekuwa yao kwa kuwashinikiza hata wasioitaka,” alisema Miraji.
Mwenyekiti huyo wa ADC alisema athari zitakazotokea katika mchakato huu zitasababisha wananchi kukosa katiba waliyoitarajia kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment