Pages

Pages

Pages

Thursday 20 February 2014

MENEJA UAJIRI KIZIMBANI KWA KUMWIBIA MWAJIRI


Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha

Meneja Mwajiri wa Kampuni ya ujenzi ya Northern Engineering Ltd ya jijini Arusha, Didier Mlawa leo amefikishwa kizimbani kwa kosa la kumwibia mwajiri akiwa mtumishi kinyume cha sheria.

Mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi, Mustapher Siyani, Wakili wa serikali, Ellen Rwijage alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa la hilo Agosti 30, mwaja jana.

Wakili Rwijage alidai kosa hilo ni kinyume cha kifungu sheria namba 271 kanuni ya adhabu ikisomwa pamoja na kifungu cha 265 sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002.

"Akiwa eneo la Mianzini jijini Arusha zilizko ofisi za kamapuni ya Northern Engineering Ltd, Mshakiwa akijua kwamba ni kosa, alimwibia mwajiri wake fedha taslimu Sh. 1 milioni kinyume cha sheria," alidai Wakili Rwijage.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na kuachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao licha kutakiwa kuwa wakazi wa Jiji la Arusha wenye kazi na anuani zinazoeleweka kila mmoja alisaini hati ya dhamana ya Sh. 1 milioni.

Upelelezi wa shauri hilo halijakamilika na limeahirishwa hadi Machi 19, mwaka huu litakapotajwa tena.

No comments:

Post a Comment