Pages

Pages

Pages

Thursday 2 January 2014

WAWILI MBARONI KWA NYARA ZA SERIKALI


Na Mussa Mwangoka, Mwananchi.

Sumbawanga. Polisi mkoani Rukwa inawashikilia watu wawili akiwemo dereva wa gari mali ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wakiwa na mizoga miwili ya nyamapori aina ya swala kinyume cha sheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda amemtaja mmoja wa watuhumiwa hao kuwa ni Innocent Sikazwe “Kajole” ambapo mtuhumiwa mwingine jina lake halikuweza kufahamika mara moja.
Kwa mujibu wa Mwaruanda, tukio hilo lilitokea juzi saa saba usiku katika Kijiji cha Nkundi wilayani Nkasi likilihusisha gari linalodaiwa kuwa mali ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa lililokuwa likiendeshwa na mtuhumiwa Sikazwe.
Inadaiwa watuhumiwa waliwinda wanyama hao katika shamba la mifugo linalomilikiwa na Dk Chrisant Mzindakaya.
“Dk Mzindakaya alitutaarifu na askari walifika kijijini hapo mara moja na kuwakamata watuhumiwa hao .
“Ndipo tulipowasiliana na maofisa wa wanyamapori ambao walithibitisha mizoga hiyo miwili ya wanyama hao kuwa ni mali ya Serikali na watuhumiwa hawakuwa na kibali chochote cha kuwinda wanyama hao,” alibainisha Mwaruanda .
Alisema walipohojiwa walikiri waliwagonga kwa bahati mbaya wanyama hao hivyo waliamua kuwapakia kwenye gari hilo. “Hii ni nyara ya Serikali kama waliwagonga walipaswa kufuata taratibu lakini haikuwa hivyo,” alisisitiza .

CHANZO: Mwananchi

No comments:

Post a Comment