Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto
UCHAGUZI
Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA),
utafanyika Februari 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Uamuzi
huo ulifikiwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya TASWA kilichofanyika
Dar es Salaam jana kujadili masuala mbalimbali ya chama na waandishi wa
habari za michezo kwa ujumla.
Kikao kilikubaliana kuwa uchaguzi ufanyike kwa katiba ya zamani, kwani mchakato wa katiba mpya unaweza kuchukua muda mrefu, hivyo kusababisha viongozi waliopo madarakani kuendelea kukalia viti kinyume cha katiba, jambo ambalo si sahihi.
Kikao kilikubaliana kuwa uchaguzi ufanyike kwa katiba ya zamani, kwani mchakato wa katiba mpya unaweza kuchukua muda mrefu, hivyo kusababisha viongozi waliopo madarakani kuendelea kukalia viti kinyume cha katiba, jambo ambalo si sahihi.
Kutokana
na hali hiyo viongozi wapya watakaochaguliwa moja ya kazi yao kubwa
itakuwa kuifanyia marekebisho makubwa katiba ya chama chetu ili iende na
wakati.
Kikao
kimekubaliana kuwa wanachama wote walipie ada zao zote wanazodaiwa
kuanzia mwaka 2011, hadi mwaka 2013, na mwisho wa kufanya hivyo ni
Januari 31 mwaka huu na yule atakayeshindwa kutekeleza agizo hilo
atapoteza haki ya kupiga kura na atahesabika si mwanachama hai.
Malipo
yafanywe kwa Mhazini Msaidizi, Mohammed Mkangara, 0658-123082 na hakuna
mwanachama mpya atakayekubaliwa kujiunga na chama mpaka baada ya
Uchaguzi Mkuu.
Pia
Kamati ya Utendaji imeunda Kamati ya Uchaguzi na kumteua Mwenyekiti wa
zamani wa TASWA, ambaye kwa sasa ni Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Kusimamia Uchaguzi Mkuu wa TASWA, ambapo pia kutakuwa na wajumbe wengine
wanne.
Wajumbe
hao ni Katibu Mkuu wa zamani wa TASWA, Mwina Kaduguda, aliyepata kuwa
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TASWA, Peter Mwenda na wanahabari
Isakwisa Mwaifuge na Mbonile Burton ambao wote ni wanachama wa TASWA.
Pia
Kamati ya Utendaji imekubaliana tuombe wawakilishi wawili wawe
waangalizi wa uchaguzi huo kuhakikisha haki sio tu inatendeka bali pia
ionekane inatendeka, ambapo mmoja atatoka Baraza la Michezo la Taifa
(BMT) na mwingine Idara ya Habari (MAELEZO), utaratibu wa kuwasiliana na
taasisi hizo mbili unaendelea.
Fomu
za kuwania uongozi zitaanza kutolewa Februari 10 hadi Februari 14 mwaka
huu saa kumi alasiri, masuala mengine yahusiyo uchaguzi huo, ikiwemo
mahali utakapofanyika yatatangazwa baada ya kikao cha sekretarieti ya
TASWA na Kamati ya Uchaguzi kitakachofanyika Februari 3.
Si dhambi wanaotaka kuongoza kutangaza nia zao mapema wakiona inafaa.
Nawasilisha.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
09/01/2014.
No comments:
Post a Comment