Pages

Pages

Pages

Tuesday 14 January 2014

MTOTO WA DARASA LA TANO ATOWEKA IRINGA

 Mtoto Cliff Moses Kilonge (10)
Mtoto Cliff Moses Kilonge (10) anayesoma darasa la tano katika shule ya msingi Ukombozi, Mtwivila katika Manispaa ya Iringa, ametoweka nyumbani na hajulikani aliko.

Inaelezwa kwamba, mtoto huyo aliondoka jana Jumatatu asubuhi akiwa amevaa sare za shule, lakini taarifa zinasema hakufika.
Juhudi za kumtafuta kila kona zimefanyika, lakini mpaka sasa hajapatikana.
Kwa yeyote atakayefanikiwa kumuona, tafadhali atoe taarifa katika kituo chochote cha polisi ama awasiliane na mama wa mtoto huyo kupitia namba 0752317759.

No comments:

Post a Comment