Leo hii nimebahatikakuwemo kwenye ziara ya wanahabari wa Mkoa wa Iringa ambao watazuru Hifadhi za taifa za Serengeti, Tarangire, Manyara, Arusha hadi Mlima Kilimanjaro.
Gari tuliyokuwa tuondoke nayo moja kwa moja ilipata hitilafu wakati tuko mjini Iringa, hivyo tukaunga na gari moja hadi Morogoro ambako tumebadilisha gari nyingine kupitia Dodoma. Kesho tutaendelea na safari kupitia Singida, Babati hadi Arusha Mjini kabla ya kuingia huko porini kuanza kucheza na wanyama mwitu.
Lengo la ziara hii ni kujifunza kwa vitendo, kwa kuona namna utalii wa ndani unavyoweza kuchangia ongezeko la pato la taifa hasa katika Nyanda za Juu Kusini ambako kwa sasa serikali ndiko ilikoweka mkazo baada ya kuona Kanda ya Kaskazini imezidi kupiga hatua.
Tunaamini ziara hii itakuwa na mafanikio.
Ndani ya kibasi kuelekea Morogoro. Hawa ni 'wasaka nyoka' wenzangu.
Na hapa tukakutana na Ritta Kabati (wa pili kulia), Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa. Wengine pichani ni madada zetu 'wasaka nyoka'.
Kabla ya kuelekea Dodoma gari yetu, no sorry gari tuliyokodishiwa, inajaza mafuta ya 'videbe'. Nimechoka mwenzenu, ndo nimeingia muda huu Makao Makuu.
Blog hii itakuletea habari mbalimbali za utalii kuanzia leo na kuendelea, kutoka katika ziara ya wanahabari wa Mkoa wa Iringa katika Hifadhi za Taifa za Serengeti, Tarangire, Manyara, Arusha hadi Mlima Kilimanjaro. Hakikisha hukosi kufuatilia.
Daniel Mbega
0784-939319
Blog hii itakuletea habari mbalimbali za utalii kuanzia leo na kuendelea, kutoka katika ziara ya wanahabari wa Mkoa wa Iringa katika Hifadhi za Taifa za Serengeti, Tarangire, Manyara, Arusha hadi Mlima Kilimanjaro. Hakikisha hukosi kufuatilia.
Daniel Mbega
0784-939319
No comments:
Post a Comment