Pages

Pages

Pages

Wednesday 11 December 2013

TUSIPOANGALIA WAZUNGU WATATUONGOZA HIFADHINI, NASI TUTAKUWA WATALII


Ndugu zangu,
Nikiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, nilifanikiwa kutengeneza marafiki wapya, kama hawa Yanik na Emmanuel Mitchell, ambao wanasema ni wazoefu wa kutembelea hifadhi za Tanzania.
Walikuwa wameandamana na baba na mama yao, dada yao na wadogo zao watatu - ni familia nzima.
Karibu wanyama wengi, ambao wewe unawasoma vitabuni na kuwaona kwenye luninga, wenzako wamewaona kwa macho.
Inashangaza kuona sisi Watanzania tunashindwa kutembelea vivutio hivi ambavyo viko kwetu, tena kwa bei nafuu kuliko wageni, na tunabaki kusimuliwa tu.
Hakika, tusipokuwa makini utafika wakati Wazungu hawa, ambao wanaanza kuupenda utalii tangu utotoni, watakuja kuwa waongoza watalii na sisi tutakuwa ndio watalii wenyewe katika nchi yetu!
Tuzinduke, twendeni tukatembelee vivutio vyetu.

Ndugu yenu,
Daniel Mbega

No comments:

Post a Comment