Pages

Pages

Pages

Wednesday 4 December 2013

TUNAKWENDA LAKE MANYARA NATIONAL PARK

Ndugu zangu,
Niko na wanahabari wenzangu kutoka Nyanda za Juu Kusini ambao tumekuja Arusha jana usiku kwa ziara ya wiki mbili ya kujifunza namna ya kuandika habari za utalii wa ndani. Kama nilivyosema juzi, tutatembelea Hifadhi za Taifa za Serengeti, Manyara, Tarangire, Arusha na kisha tutapandisha Mlima Kilimanjaro.
Hivi sasa, baada ya muda mfupi ujao, tutaanza safari ya kuelekea Hifadhi ya Ziwa Manyara, ambako huko kuna simba pekee wanaokwea miti kama chuo, kama picha inavyoonyesha.
Lakini tutaona Korongo wengi kama hawa pamoja na wanyama aina ya Kiboko.
Hakikisha hukosi kufuatilia blog hii kupata habari za kina za utalii zinazotokana na ziara hii ambayo imedhaminiwa na Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA).

Daniel Mbega

No comments:

Post a Comment