Pages

Pages

Pages

Monday 30 December 2013

MSIMU WA KILIMO HUU, NALIMA MWENYEWE

 Mwenzenu nilisamehe Krismasi nikaenda shambani kulima. Naamini hii nayo ilikuwa ibada, maana ni vyema watoto wakagombea mlango wa chooni ili waisherehekee vyema sikukuu. Hata kama kashamba kadogo, kananitosha.

 Mvua zenyewe hizi za mang'amung'amu, bila taimingi unaweza kuvuna mabua. Mungu atusamehe nyakati nyingine.
 Haya ni mambo ya kawaida, lazima kuweka grisi kwenye chombo ili kulainisha mitambo. 
 Naam. Ndilo shamba langu hili, ninapowaambia nimekuwa mkulima mdogo watu hawaamini.
 
Kazi inaendelea. Yakiiva nitawaalika. Nimepanda mahindi na maharagwe. Karibu Iringa wadau.

No comments:

Post a Comment