Pages

Pages

Pages

Sunday 1 December 2013

MKWARA UNASAIDIA, HAKUNA 'KUCHIMBA DAWA' PORINI...

Hapa ni mwendo mfupi tu kabla ya kuingia Makambako ukiwa unatokea Iringa. Miaka mitatu iliyopita eneo hili lilikuwa halitamaniki kabisa kwa harufu kali kutokana na abiria wengi 'kulitumia kuchimba dawa'. Watu walikuwa wakizama vichakani kujihifadhi. Lakini baada ya mkwara mzito wa Waziri wa Uchukuzi, Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwamba kuanzia Septemba 2012 hakuna abiria kuchimba dawa porini badala yake madereva wa mabasi wasimame sehemu zenye vyoo, halmashauri husika pamoja na wanajamii wameweza kufyeka vichaka hivyo na kujenga vyoo, ambavyo abiria hawatozwi hata senti tano. Hongera Magufuli, punda haendi bila viboko...

 

Na bidhaa ziko tele...

No comments:

Post a Comment