Pages

Pages

Pages

Monday 18 November 2013

UNATAKA KWENDA MBINGUNI?

Mchungaji Chavalla alikwenda kwenye baa moja mjini Iringa na kumwendea jamaa wa kwanza aliyemuona akigida pombe. "Unataka kwenda mbinguni?" akamuuliza jamaa huyo, ambaye naye alijibu, "Ndiyo, Baba Mchungaji, nataka kwenda." Mchungaji akasema, "Kwa jina la Mungu, ondoka kwenye baa hii sasa hivi."

Kisha akamwendea jamaa mwingine, "Unataka kwenda Mbinguni, kijana wangu?" Na jamaa akajibu, "Ndiyo, Mchungaji, hakika nataka kwenda Mbinguni." Mchungaji akamwamuru, "Basi ondoka kwenye baa hii sasa hivi!"

Mchungaji Chavalla akaendelea na zoezi hilo kwenye baa yote mpaka alipokutana na jamaa wa mwisho. "Unataka kwenda Mbinguni, mpendwa?" akauliza, Jamaa akaitazama chupa yake ya bia iliyokuwa nusu, akageuka na kumtazama Mchungaji, halafu akasema, "Hapana, sitaki kwenda Mchungaji."

"Unataka kuniambia, kijana, kwamba utakapokufa, hutaki kwenda Mbinguni?" Mchungaji Chavalla akauliza kwa mshangao. 

"Anhaa, sawa, nitakapokufa, sawa Mchungaji, ninataka kwenda Mbinguni. Nilidhani ndiyo kwanza ulikuwa unawakusanya watu ili waende sasa hivi!"

No comments:

Post a Comment