Pages

Pages

Pages

Wednesday 6 November 2013

NAPE ATIMIZA AHADI KWA WANANCHI WA NYAMONGO

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifafanua jambo wakati wa kikao maalum cha ndani na wakazi wa eneo la Nyamongo, ambapo wananchi wa eneo hilo walikuwa wakieleza kero zao na wamiliki wa mgodi wa North Mara.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Ndugu John Henjewele akiwaelezea wakazi wa Nyamongo kazi za kikosi kazi (Task force) katika kurahisisha shughuli za kutathimini ardhi na kuchukua malalamiko ya wananchi dhidi ya wawekezaji wa mgodi wa North Mara.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiangalia moja ya eneo linaloaminika kutiririsha maji yenye kemikali kutoka kwenye Mgodi wa North Mara kwenda kwenye mto Mara na kuhatarisha afya za wananchi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia kwa karibu kabisa maji ya kemikali kutoka machimbo ya mgodi wa North Mara kuelekea mtoni.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma jiwe la msingi la ofisi ya Kikundi cha Bodaboda Nyamongo mara baada ya kuzindua ofisi hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Ndugu Amos Sagara Nyabikwi akihutubia wakazi wa Nyamongo wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliwaelezea wananchi wa eneo hilo hatua za awali za kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao zilivyoanza.

No comments:

Post a Comment