Pages

Pages

Pages

Monday 14 October 2013

MWENGE UMEZIMWA IRINGA

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Mwenge wa Uhuru mjini Iringa leo.
Luteni Alexander Nyirenda akikabidhiwa Bendera ya Taifa na Mwalimu Nyerere mwaka 1961.
Nyirenda akiwa na Mwenge wa Uhuru.
Luteni Nyirenda akipandisha Bendera ya Taifa pamoja na Mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro Desemba 9, 1961.

 Hapa ni wakati amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya mauti kumfika mwaka 2008.


"Tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro ili uangaze nje ya mipaka yetu, ulete matumaini pasipo na matumaini, upendo penye chuki, na heshima mahali palipo na dharau."

Sisi tunataka kuwasha mwenge
Na kuuweka juu ya mlima
Mlima Kilimanjaro

Kuwasha mwenge x 2
Na kuuweka Kilimanjaro
Umulike hata nje ya mipaka yetu
Ulete tumaini
Pale ambapo hapana matumaini

Hatimaye Mwenge wa Uhuru umefikia kilele chake leo hii kwenye Uwanja wa Samora baada ya kuzimwa rasmi na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Dk. Jakaya Mrisho Kwete.

Mwenge wa Uhuru ni mojawapo ya Alama za Taifa la Tanzania. Ndio mwanga wa uhuru tunaojivunia kwani uliwashwa usiku ule wa Desemba 9, 1961 kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro na Luteni Kanali Alexander Donald Gwebe Nyirenda.Kila mwaka Mwenge wa Uhuru unakimbizwa nchini kote kusambaza ujumbe wa matumaini, upendo, heshima na amani na hufikia kilele chake Oktoba 14 ili kukumbuka kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Pamoja na kuwa na ujumbe maalum kila mwaka, lakini mbio za mwenge hutumika kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Kwa mwaka 2012 zaidi ya miradi 270 ya maendeleo yenye thamani ya TShs.158.837 bilioni ilizinduliwa na katika mbio hizo wananchi walichangia jumla ya TShs. 11.5 bilioni kwa ajili ya kukamilisha baadhi ya miradi.
Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ndiye aliyeuwasha Mwenge huko Chokocho, Wilaya ya Mkoani katika Mkoa wa Kusini Pemba mnamo Mei 6, 2013.
Rais kwa Watanzania wenzangu, tuendelee kudumisha Tunu za Taifa.
 

No comments:

Post a Comment