Pages

Pages

Pages

Monday 28 October 2013

MANISPAA YA ILALA KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA


Ofisa Uhusiano kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu (kulia) akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) mafanikio yaliyopatikana katika utoaji wa huduma ya afya ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya afya katika manispaa hiyo, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dk. Asha Mahita.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dk. Asha Mahita (kushoto) akitoa tahadhari kwa wananchi kupitia waandishi wa habari (hawapo pichani) kuacha tabia ya kufungua makaro ya maji machafu kipindi cha mvua ili kuepuka magonjwa ya mlipuko, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Manispaa hiyo Bi. Tabu Shaibu. Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

No comments:

Post a Comment