Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 8 March 2016

WAFANYAKAZI WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WATOA MSAADA HOSPITALI YA MWANANYAMALA KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Meneja wa PPF Kanda ya Kinondoni, Zahra Kayugwa (kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali mzazi aliyejifungua mtoto wa Kiume, Hospitali ya Mwananyama, Joyce Lucas, mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam, wakati Wafanyakazi wa Mfuko huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo Machi 8, 2016. Picha na Mafoto Blog.

Meneja wa PPF Kanda ya Kinondoni, Zahra Kayugwa (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa wazazi waliokuwa wamelazwa kweye Wodi ya Watoto wachanga/Njiti  katika  Hospitali ya Mwananyama, wakati Wafanyakazi wa Mfuko huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo Machi 8, 2016. Picha na Mafoto Blog.
Meneja wa PPF Kanda ya Kinondoni, Zahra Kayugwa (kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali mgonjwa mzazi aliyelazwa kwenye Wodi ya kina mama waliofanyiwa upasuaji Hospitali ya Mwananyama, jijini Dar es Salaam, wakati Wafanyakazi wa Mfuko huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo Machi 8, 2016. Picha na Mafoto Blog.
Meneja wa PPF Kanda ya Kinondoni, Zahra Kayugwa (katikati) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali Caroline Hanne Van, Raia wa Denmark kwa niaba ya watoto wawili (kitandani) waliodaiwa kuokotwa jana maeneo ya Mbezi Beach na kufikishwa hospitalini hapo leo asubuhi, wakati Wafanyakazi wa Mfuko huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo Machi 8, 2016. Kushoto ni Emel Kudahl Christensen na wa tatu (kulia aliyekaa) ni Emma Nikoline Wennberg, wauguzi wa kujitolea kutoka nchini Denmark. Picha na Mafoto Blog.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakigawa vitu mbalimbali kwa wagonjwa wazazi waliolazwa kwenye Wodi ya Watoto wachanga/Njiti, wakati Wafanyakazi wa Mfuko huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo Machi 8, 2016. Picha na Mafoto Blog.

No comments:

Post a Comment