Na Beatrice Lyimo-Dar es salaam
Mwenyekiti wa Chama
cha Mapinduzi (CCM) na Rais mstaafu wa
awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Mhe. Truong Tan Sang katika
ofisi ndogo za Makao makuu ya Chama cha Mapinduzi mtaa wa Lumumba jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza mara baada
ya mapokezi ya Rais huyo, Dkt.
Kikwete amesema kuwa lengo la ujio wa Rais wa wa Vietnam katika ofisi za CCM ni
kudumisha na kuendeleza uhusiano wa
kihistoria uliopo kati ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) na Chama cha Komunisti cha Vietnam.
Amesema Chama cha cha
Komunisti cha Vietnam na chama cha TANU na ASP vimekuwa na mahusiano ya muda mrefu ya kihistoria toka kipindi ambacho vietnam ilikua ikipambana na ubeberu
wa kimarekani.
Ameeleza kuwa katika mapambano hayo Chama cha TANU kiliunga mkono juhudi hizo kwa kuwaunga mkono wananchi wa Vietnam katika ukusanyaji
wa michango mbalimbali iliyowezesha mapambano dhidi ya Ubeberu wa Kimarekani.
Aidha, amebainisha
kuwa ujio wa Rais huyo wa Vietnam kama kiongozi wa Mkuu wa Chama na Serikali katika
ofisi ndogo za Makao makuu ya CCM ni ishara
ya kudumisha uhusiano mzuri uliopo baina ya vyama hivyo viwili ambavyo viko madarakani.
No comments:
Post a Comment