Mfanyakazi wa Kituo cha Biashara cha Kimataifa (WTC) akiingia ofisini jana Jumatatu.
Miaka 13 baada ya majengo ya awali ya Kituo cha Biashara cha Kimataifa, WTO kuharibiwa katika shambulio la kigaidi la Septemba 11, 2001, kituo hicho kilichopo jijini New York kimefunguliwa kwa shughuli za biashara.
Waajiriwa katika kampuni kubwa ya uchapishaji ya Conde Nast wameanza kuingia katika jengo hilo la One World Trade Centre lenye urefu wa ghorofa 104.
Jengo hilo lenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 3.8 limechukua muda miaka nane kulijenga na kwa sasa ndilo jengo refu kuliko yote nchini Marekani.
Limekodishwa kwa asilimia 60% na taasisi ya serikali ya Marekani ya Utawala wa Huduma imeingia mkataba wa kuchukua eneo la futi za mraba 275,000.
"Mwonekano wa angani wa jiji la New York umerejea tena," anasema Patrick Foye, mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Bandari, ambayo yanamiliki eneo hilo lililorejeshewa hali yake.
Jengo hilo lenye urefu wa mita 541 kwenda juu liko katikati ya eneo hili, ikiwemo sehemu ya eneo la kumbukumbu la majengo ya zamani na makumbusho yaliyofunguliwa mwaka huu.
Eneo la kubarizi juu ya jengo hili hatimaye litakuwa wazi kwa matumizi ya umma.
Jengo hili la One World Trade Center kwa sasa linatawala anga la eneo la Manhtattan kwa kuonekana juu ya majengo mengine.
Baadhi ya watu wamezungumzia uzuri wa jengo hili.
Wafanyakazi wapatao 170 wa kampuni ya Conde Nast watakuwa wamehamia katika jengo hili wiki hii, fwakijaza ghorofa tano. Wafanyakazi wapatao 3,000 zaidi watajiunga na wenzano ifikapo mapema mwaka 2015.
Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya bandari Bwana Foye ameongeza kuwa jengo hili ndilo "jengo lenye usalama zaidi nchini Marekani".
TJ Gottesdiener wa kampuni ya Skidmore, Owings & Merrill ambayo ilitoa mchoro wa mwisho wa jengo hili amesema jengo hili limevuka mfumo wa majengo yaliyopo jijini New York na limejengwa na kuimarishwa kwa zege la chuma cha pua.
Eneo la jengo hili la One WTC pia imekodishwa kwa kampuni ya matangazo ya Kids Creative, GSA, na futi za mraba 191,000 zimekodishwa kwa kampuni ya China, ambayo inajishughulisha na masuala ya biashara na utamaduni.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment