JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LATANZANIA
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MKUTANO WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
TAHERE 4 – 28 NOVEMBA, 2014 – DODOMA
Kufuatia
uwepo wa Bunge Maalum la Katiba lililomalizika mwezi Oktoba, Mkutano wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa
Kumi na Sita na wa Kumi na Saba ilipangwa kufanyika kwa pamoja kuanzia tarehe 4
– 28 Novemba, 2014 mjini Dodoma.
Kazi
zitakazofanyika katika mikutano hiyo ni pamoja na Bunge kukaa kama Kamati ya
Mipango kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 94(1) na kupokea, kujadili na kutoa
maoni na ushauri kuhusu bajeti ya serikali, vyanzo vya mapato pamoja na
mapendekezo ya utekelezaji wake. Aidha kutakuwa na kusomwa kwa mara ya pili na
hatua zake zote kwa miswada ya Sheria ya Serikali ambayo ilikwishasomwa kwa mara ya kwanza
katika mikutano iliyotangulia; Muswada Binafsi wa Mbunge na Muswada Binafsi wa
Kamati kama ifuatavyo:
A.
Miswada ya Sheria ya Serikali
i.
Muswada ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani
wa Mwaka 2014. [The Value Added Tax Bill,
2014]
ii.
Muswada wa Sheria ya Takwimu wa Mwaka 2013. [The Statistics Bill, 2013].
iv.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta
Binafsi wa Mwaka 2014 [The Public
Private Partnership (Amendment) Bill, 2014]
na,
v.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria
mbalimbali wa Mwaka 2014. [The Written Laws (Miscellaneous
Amendments) Bill, 2014]
B.
Muswada Binafsi wa Mbunge
Muswada wa Sheria ya
Baraza la Vijana wa Mwaka 2013. [The Youth Council Bill, 2013]
C.
Muswada Binafsi wa Kamati
Muswada wa Sheria ya
Bajeti wa Mwaka 2014. [The Budget Bill, 2014].
Aidha,
Bunge litapokea taarifa ya Kamati Teule iliyoundwa tarehe 1/11/2013 ili
kuchunguza na kuchambua sera mbalimbali zinazohusu masuala ya ardhi, kilimo,
mifugo, maji na uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya ardhi.
Pamoja na mambo mengine, Bunge pia
litajadili maazimio matatu ambayo ni:
i.
Azimio la kuridhia Itifaki ya Afrika
Mashariki Kuhusu Ushirikiano katika Masuala ya Kiulizi. [The East African Protocol on Cooperation in Defence Affairs].
ii.
Azimio la Bunge kuhusu mapendekezo ya kuridhia
makubaliano ya msingi ya Ushirikiano katika Bonde la Mto Nile, [Agreement on the Nile River Basin
Co-operative Framework – CFA]; na
iii.
Azimio la kuridhia Itifaki ya Uzuiaji wa
Vitendo Haramu dhidi ya Usalama wa Miundombinu ya kudumu iliyojengwa chini ya
Bahari katika mwambao wa Bara ya mwaka 1988. [The Protocol for the Suppression of Unlawful Acts against the Safety
of Fixed Platforms located on the Continental Shelf – SUA, 1988].
Aidha, kutakuwa na maswali ya kawaida kwa mujibu wa kanuni ya
39(1) ambapo kwa mikutano hii miwili yakuwa 265 na maswali kwa Waziri Mkuu kwa mujibu wa kanuni
ya 38(1).
Mwisho
Waheshimiwa Wabunge wakiwa Dodoma watapata fursa ya kushiriki semina mbalimbali
za kujenga uwezo katika nyanja za kilimo na usalama wa chakula; faida za
ushirikiano katika Bonde la Mto Nile; na umuhimu wa kupima/kuchunguza afya mara
kwa mara.
Ratiba
ya Mkutano itatolewa mara baada ya kikao cha Kamati ya Uongozi kitakachofanyika
tarehe 4 Novemba 2014, Dodoma.
Imetolewa na Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam,
30 Oktoba 2014
No comments:
Post a Comment