Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis (katikati) akiwa na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina (kushoto) na Rais wa Israel, Shimon Peres leo hii huko Vatican ambako wawili hao wamekwenda kuomba amani Mashariki ya Kati.
Papa Francis amewapokea viongozi wa Israil na Palestina katika Vatikani.
Rais Shimon Peres wa Israel na Mahmoud Abbas wa Palestina walikutana Vatican kuomba amani Mashariki ya Kati.Viongozi hao wawili walikutana na Papa nje ya nyumba yake, kabla ya kusafiri pamoja naye na kiongozi wa kanisa la Orthodox, Askofu Mkuu Bartholomew, hadi kwenye sherehe katika bustani ya Vatican. Wakitarajiwa kupandisha mzaituni kama alama ya kudumu ya hamu ya pande zote mbili ya kupata amani baina ya watu wa Israil na Palestina.
Papa alisema yeye hataki kuhusika moja-kwa-moja na mazungumzo ya amani, lakini anatumai viongozi hao wakikutana, huenda ikasaidia kupunguza uhasama kati yao.
BBC
No comments:
Post a Comment