Abdel-Fattah al-Sisi
ameapishwa kuwa rais mpya wa Misri katika seherehe iliyofanywa kwenye
mahakama makuu ya katiba mjini Cairo.
Kiongozi wa muda, Adly Mansour na Bwana al-Sisi walitia saini waraka wa kukabidhi madaraka kwake rais mpya - kwa mara ya kwanza katika historia ya Misri.
Rais mpya alisema hilo ni tukio la kihistoria.
Mkuu huyo wa zamani wa jeshi alishinda katika uchaguzi wa mwezi uliopita kwa asili-mia-97, ingawa upinzani ulisusia uchaguzi huo.
Wafuasi wa Rais al-Sisi walisherehekea katika medani ya Tahrir mjini Cairo.
Mfuasi mmoja wa al-Sisi, Fakhri Gamel Abdul Khaleq, alisema anatumai sherehe za leo ndio zitamaliza matatizo yaliyopita:
"nampongeza Bwana rais anapoapishwa leo.
Mungu ajaalie uwe mwaka wa furaha kwetu na kwa Wamisri wote.
Na tunaomba Mungu atunusuru na yale yaliyotokea kabla, na tutakuwa watu wema.
Mungu akipenda, kama alivosema rais, tutakuwa mfano mzuri wa ustaarabu".
BBC
No comments:
Post a Comment