Kiongozi wa Kanisa
Katoliki Papa Francis amewakaribisha Rais wa Israil, Shimon Peres, na mwenzake
kutoka Palestina, Mahmoud Abbas, katika maombi ya aina ya kipekee katika makao
makuu ya Kanisa Katoliki ya Vatican. Viongozi hao wawili walikutana na Papa nje
ya makaazi yake kabla ya kuandamana naye, wakiandamana na kiongozi wa Kanisa la
Ordhodoz, Partriarch Artholomew kwa hafula maalumu katika Medani ya Vatican.
Akiongea katika hafula hiyo Papa alisema ujasiri na nguvu vinahitjika katika
juhudi za kuleta amani.
"Kuleta amani
kunahitji ujasiri mkubwa kuliko vita. Kunahitaji ujasiri wa kusema ndio kwa
mkutano na La kwa vita; ndio kwa mashauriano na La kwa makabiliano; ndio kwa
kuheshimu mikataba na La kwa uchokozi; Ndio kwa ukweli na La kwa Uongo; kwa
haya yote tunahitaji ujasiri na nguvu moyoni," Papa alisema
Na katika hotuba yake
Bwana Peres alisema alitakia vizazi vyote vijavyo amani ya kudumu:
"Rafiki wapenzi, Nilikuwa mchanga, na sasa nimezeeka. Nilishuhudia vita,
Nilionja amani. Sitawahi kusahau familia zilizofiwa, wazazi na watoto
waliolipia gharama kubwa kwa vita hivyo. Na maisha yangu yote sitakoma kuitisha
amani, kwa niaba ya vizazi vijavyo. Naomba sisi sote tuuungani mikono na
kufurahi kwa sababu ni wajibu wetu kufanya hivyo kwa niaba ya watoto wetu.
Na kwa upande wake
Bwana Abbas aliombea amani katika mkutano huo," alisema Peres.
Naye kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas, aliomba kwenye hafula hiyo.
"Ee Bwana, tuletee amani ya kudumu na ya haki katika taifa letu na eneo
letu, kwa ujumla, ili watu wetu na watu wote wa Mashariki ya Kati na Dunia
nzima ifurahie matunda ya amani, utangamano na kuishi kwa pamoja kwa upendo.
Baada ya sherehe hiyo,
iliyoshirikisha maombi ya Kikristo, Kiyahudi na Kiislamu, waliokuwepo
walisalimiana kwa mikono na kupanda Mzaituni katika Medani ya Vatican kama
ishara ya amani.
Papa ametangaza
hadharani kuwa hataki kuingilia moja kwa moja mashauriano ya amani ya Mashariki
ya kati, yaliyoporomoka Aprili lakini akasema kuwa anatarajia kwamba mkutano
katika Vatican utapunguza uahasama kati ya pande hizo mbili kinzani za
Mashariki ya Kati.
CHANZO, BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment