Pages

Pages

Pages

Wednesday, 2 February 2022

RASILIMALI TELE LAKINI CCM INALIA UMASKINI

 

Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza

Na Daniel Mbega

HADI kufikia Juni 2020 thamani ya mali za Chama cha Maoinduzi (CCM) ilikuwa imepanda huku mapato yake yakifikia Sh. 59.8 bilioni kwa mwezi.

Ongezeko hilo yalikuwa ni matunda ya uhakiki wa mali za Chama, kwani kabla ya zoezi hilo chama hicho kilikuwa kikiingiza mapato ya Sh. 191 bilioni kwa mwaka huku mali nyingi zikiwa chini ya watu wachache, hali iliyokifanya chama kuwa maskini na hoi kiuchumi na kuwa ombaomba licha ya kuwa na rasilimali nyingi.