Pages

Pages

Pages

Thursday 2 January 2014

MINZIRO: SITISHWI NA YANGA

Fred Felix Isaya Kataraiya 'Minziro'

ALIYEKUWA kocha msaidizi wa klabu ya Yanga, Fredy Felix Minziro, amesema kwamba hatishwi na uamuzi wa kuachwa kwake katika benchi la ufundi la timu hiyo, kwa sababu ana ujuzi wa kuupeleka sehemu nyingine. 
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Minziro alisema amekuwa akivuna ujuzi mwingi kutoka kwa makocha mbalimbali waliopita Yanga katika kipindi cha miaka minne, huku akiwa kama kocha msaidizi.
Alisema jambo hilo linampa matumaini makubwa kuwa uwezo wake umekuwa mkubwa na hawezi kukosa timu ya kuifundisha atakapoona inafaa, hivyo hana shaka na uamuzi wa mabosi wake.
“Siwezi kuumizwa na hatua hii ya kuachwa Yanga, ukizingatia kuwa sijaona tatizo langu wala kupewa sababu ya kueleweka kwa nini benchi la ufundi linavunjwa bila sababu za msingi.
“Hata hivyo kwa kuwa wao ndio wameamua, nimepokea uamuzi huo na nitakapoamua kusaka timu ya kufundisha siwezi kukosa kutokana na ujuzi wangu nilionao,” alisema Minziro.
Yanga imevunjwa benchi lake la ufundi baada ya awali kumtimua kocha wake mkuu, Ernest Brandts na baadaye kuamua kutoshiriki Kombe la Mapinduzi, lililoanza jana visiwani Zanzibar.

CHANZO: Mtanzania

No comments:

Post a Comment